Bonde la Mto Mara, ni mto unaopatikana baina ya nchi ya Kenya na Tanzania eneo lenye wakazi takribani milioni 1.3. Chanzo cha Mto Mara ni Msitu wa Mau nchini Kenya na mto huu humwaga maji yake katika Ziwa Victoria. Takribani asilimia 65 ya mto huu ipo Kenya na 35 iliyosalia inapatikana Tanzania. Baina ya Ziwa Victoria na Msitu wa Mau, mto mara unapita katika hifadhi za Masai Mara, na Serengeti inayo unda bonde la Serengeti na Mara eneo maarufu duniani la wanyama wanaohama wakati wa mabadiliko ya misimu. Eneo la Mradi wa SELVA ni sehemu ya kusini yaani eneo la Tanzania. Hii huhusisha hifadhi ya mbuga ya SERENGETI, jamii kadhaa namakazi ya watu baina ya hifadhi na Ziwa Victoria, ikihusisha maeneo chepe, viwanda vya kimataifa, kilimo asilia, utalii na uvuvi.
Mara ni sehemu ya bonde la Mto Nile mkuu, na ndio pekee wa kudumu katika eneo la Serengeti –Mara. Eneo hili kwa sasa lipo hatarini kutokana mabadiliko ya hali ya hewa na shughuli za binadamu zinazobadili hali ya mto huo. Kwa upande mwingine jamii ya binadamu na viumbe wengine pia, wanaweza kubadilika sana kutokana na mabadiliko katika chanzo hiki muhimu cha maji.
HIfadhi ya Maandiko ya Mto Mara inawezesha upatikanaji wa habari za viumbe hai, na habari za kijamii, Makala za kitaaluma, mikataba, makala maalum, picha, ramani, ripoti, data na taswira mbalimbali zinazohusiana na eneo la karibu na Mto Mara, Afrika ya Mashariki. Hifadhi hii inahusisha habari za zamani na za sasa. http://dpanther.fiu.edu/dPanther/collections/Mara
Hifadhi ya awali inatunzwa kwa ushirikiano wa MaMaSe na SELVA. Matokeo ni hifadhi data inayoruhusu utafutaji habari ya Mto Mara na mengine yanayohusu usalama wa maji. Kama una mchango wowote katika hifadhidata hii wasiliana nasi kwa barua pepe mara@fiu.edu.
Tovuti ifuatayo, itakuunganisha na hifadhidata huru ya habari za kijiografia zilizokusanywa na MaMaSe na SELVA:
SELVA imetegesha idadi kubwa ya vifaa vya gharama nafuu katika eneo la chini la Mto Mara. Utiririkaji wa maji na mabadiliko ya halijoto naweza kuangaliwa hapa.