Mpango

Image_Mission

Dhumuni la mradi wa SELVA ni kushughulikia tatizo la usalama wa maji na changamoto zinazababishwa na shughuli za binadamu katika eneo la bonde la Mto Mara. Bondo la Mto mara, ni mali asili inayopatikana katika mataifa ya Kenya na Tanzania. Hata hivyo, mpaka sasa, sehemu kubwa ya utafiki imefanyika katika eneo la Kaskazini yaani upande wan chi ya Kenya. Mradi huu utatazama zaidi eneo la kusini la bonde la Mto Mara linalojumuisha maeneo ya mbuga ya Serengeti, Eneo chepe la Mara, na ukanda wa ziwa Victoria. Mto Mara unapatikana katika eneo muhimu sana la bayoanuwai duniani na mto huo unalisha jamii zenye tamaduni nyingi zaidi duniani. Upatikanaji wa maji safi ni jambo la muhimu sana kwa mazingira na uhai wa binadamu, uchumi, mila na tamaduni pia. Usalama wa maji safi unazidi kuhatarishwa na shughuli za maendeleo ya binadamu pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mradi wa SELVA utatengeneza jukwaa la ushirikiano katika upande wa Tanzania, nautaongoza juhudi za kupanua uelewa na kusimamia matumizi ya maji katika mazingira ya bonde la mto Mara, na wakazi wake sasa na baadaye. Mradi wa SELVA unaunga mkono juhudi zilizofanyika Kenya ili kuushughilikia mto Mara kama mto mmoja na mradi utashirikiana na miradi mingine ili kukuza ushirikiano baina ya wadau wa Kenya na Tanzania ili kuboresha usimamizi wake.

Bonde la mto mara kwa sasa ni moja kati ya maeneo ya dunia yanayobadilika kwa haraka sana, wakati huo upatikanaji wa maji safi kwa binadamu na viumbe hai wengine ni jambo la muhimu sana katika mabadiliko haya. Bonde la Mto Mara linawakilisha jamii kubwa inayopatikana katika sehemu kubwa ya eneo la bara la Afrika, mimea mbalimbali ya nchi kavu na majini, ambayo uhai wake unahatarishwa na shughuli za binadamu, mabadiliko unyeshaji wa mvua pamoja na halijoto vinavyosababishwa na kilimo cha umwgiliaji, ongezeko la uvunaji wa maji unaohusisha uchimbaji wa madini, mabwawa ya kufua umeme, na ongezeko la idadi ya watu. Kila moja kati ya shughuli hizi, kwa namna moja au nyingine, inaathiri uwepo na upatikanaji wa masi safi katika Mto Mara.

Mradi wa SELVA umewezesha na msaada toka mfuko wa MacArthur Foundation. Kwa maelezo zaidi tazama: Conservation & Sustainable Development Strategy.